
CHAMPIONZ LIGI, UCL.
Mara ya mwisho kukutana kwa Timu hizi kwenye Michuano ya Ulaya ni Mwaka 2010 wakati Bayern Munich ilipoitoa Man United kwenye Robo Fainali kwa Bao za Ugenini.Safari hii, hali ipo tofauti kwani Man United
wanaingia kwenye Mechi hii huku Wachambuzi wengi hawawapi matumaini makubwa ya kufanya
viziru dhidi ya Bayern Munich inayosifiwa kuwa ndio Timu Bora Ulaya hivi sasa na Juzi ilitwaa
tena Ubingwa wa Germany huku wakiwa na Mechi 7 mkononi wakati Man United wanasuasua kwenye Ligi Kuu England wakiwa
Nafasi ya 7.
DONDOO MUHIMU:
-ARJEN ROBBEN: “Ukizubaa Sekunde tu,utafungwa na Man United!!”Hata hivyo, licha ya Bayern kutisha kwa kufungwa Mechi mbili tu Msimu huu, moja ikiwa kwenye German Super Cup, Bayern wamekuwa na wakati mgumu na Timu za England kwani,kwenye UCL walipigwa Bao 3-2 na Man City Mwezi Desemba kwenye Mechi ya Kundi lao na vile
vile,Arsenal waliweza kutoka Sare ya Bao 1-1 na Bayern hapo Machi 11 katika Raundi iliyopita kwenye Mechi iliyochezwa Allianz Arena Jiijini Munich.
Bayern watatinga kwenye Mechi hii bila ya Kiungo wao Thiago Alcantara ambae ni Majeruhi na Man United itawakosa Mshambuliaji wao
hatari alieumia, Robin van Persie, na pia Patrice Evra ambae yuko Kifungoni kwa Mechi hii.Nae
Nyota wa Bayern, Arjen Robben, ameonya kuwa Man United wanao uwezo kuiadhibu Bayern.Robben
ya UCL baada kufunga Bao Dakika za mwisho na kuipa Bayern Bao la Pili katika Mechi ya Marudiano waliyofungwa 3-2 lakini wakasonga kwa Bao za Ugenini kwa vile Jumla ya Mabao
ilikuwa 4-4 baada ya wao kushinda Mechi ya Kwanza kwao kwa Bao 2-1.
amesema: “Litakuwa pambano kali na lazima tuchunge! Wanahabari na Wadau wana maoni kuwa Man United haipo kwenye hali nzuri na sisi tutaenda Nusu Fainali, mie sipendi hilo!”Aliongeza: “Ukizubaa Sekunde tu, utafungwa na Man United!!”Msimu wa 2009/10 Arken Robben ndie aliiwezesha Bayern Munich kutinga Nusu Fainali
No comments:
Post a Comment