SHOMARY Kapombe amejiunga na klabu ya Azam FC kufanya mazoezi ili kujiweka fiti kwa
wakati huu ambao hana timu baada ya kugoma kurejea klabu yake ya Daraja
la Nne Ufaransa, AS Cannes.Tovuti ya Azam FC imemnkukuu Kapombe
akisema kwamba ameamua kuja kufanya Azam
FC kwa sababu kwanza ni jirani na eneo
analoishi na pia wana vifaa vyote vya vya
mazoezi vitakavyosaidia kumuweka fiti.
Hata hivyo, Kapombe hakutaka kuzama ndani
juu ya mustakabali wake wa baadaye
, akisema;
“Nimekuja Azam kufanya mazoezi kujiweka fiti
tu, basi,”alisema.
Tayari kuna habari kwamba, Kapombe anataka
kucheza klabu ya Tanzania ambayo itashiriki
michuano ya Afrika mwakani.
Kiungo huyo anayeweza kucheza nafasi za
ulinzi pia, anamaliza Mkataba wake Simba SC
mwezi huu, lakini alikwishaingia Mkataba wa
miaka minne na AS Cannes ya Ufaransa mwaka
jana.
Na Simba SC imekubaliana na klabu ya Daraja
la Nne Ufaransa, kuununua Mkataba wa
mchezaji huyo arejee kufanya kazi Msimbazi
baada ya kushindwa kuendelea kucheza Ulaya.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC,
Zacharia Hans Poppe alizungumza na AS
Cannes mwezi uliopita na kufikia makubaliano
ya kuuziana Mkataba huo, ili Kapombe arejee
Msikmbazi.
Poppe alisema kwamba Simba SC imekubali
kuilipa Cannes kiasi cha Euro 33, 000 ambazo
sawa na Sh. Milioni 66 ili kurejeshewa
mchezaji wake huyo.
Kapombe alitolewa bure kwenda AS Cannes
katikati ya mwaka jana akiwa bado ana
Mkataba na klabu hiyo ya Msimbazi,
unaomalizika Aprili mwaka huu.
Baada ya kuwa Ufaransa kwa zaidi ya miezi
mitatu, Kapombe alirejea nchini Novemba
mwaka jana kwa ruhusa maalum ya kuja
kuichezea timu ya taifa katika mchezo wa
kirafiki dhidi ya Zimbabwe.
Baada ya mchezo huo, mchezaji huyo akaamua
kubaki moja kwa moja nyumbani akidai
halipwi mishahara.
No comments:
Post a Comment