Wednesday, April 2, 2014

GUARDIOLA AMUWAKIA ILE MBAYA ROONEY NA REFA...ASEMA SCHWEINSTEIGER NA MARTINEZ NI KUBWA KWAO


KOCHA wa Bayern Munich amemshutumu
Wayne Rooney kwa kujirusha na kumponza
Bastian Schweinsteiger atolewe nje kwa kadi
nyekundu usiku wa jana Manchester United
wakiweka hai matumaini ya kuendelea na Ligi
ya Mabingwa Ulaya.
Schweinsteiger pamoja na mchezaji mwenzake,
Javi Martinez wataikosa mechi ya marudiano
Jumatano ijayo nchini Ujerumani baada ya
Robo Fainali ya kwanza kumalizika kwa sare ya
1-1 jana
.
Wakati Schweinsteiger akimnyooshea kidole
Rooney aliyekuwa ameanguka chini, kocha wa
Bayern, Pep Guardiola alionekana
kumuonyesha ishara ya kujirusha refa
Mspanyola, Carlos Velasco Carballo na
baadaye akasema hajakubaliana na uamuzi
huo. "Hapana kabisa," alisema Guardiola.
Amejirusha huyoo: Guardiola akilalamikia
Rooney kuanguka kiulaini
Ameenda chini: Bastian Schweinsteiger
alimchezea rafu Wayne Rooney na kutolewa nje
kwa kadi nyekundu
Anaenda chini: Schweinsteiger akimkwatua
Rooney
Siyo vizuri babu: Schweinsteiger akimnyooshea
kidole Rooney kumtuhumu kujirusha
Sijapenda kabisa: Schweinsteiger akimlalamikia
Rooney
"Ni pigo. Hao ni wachezaji muhimu sana
kwetu. Tutajaribu kwenda Nusu Fainali, kisha
watacheza,".
Tukio hilo lilikuja baada ya David Moyes
kumuonya Carballo kabla ya mchezo huo awe
makini na mbinu za Bayern kujirusha.
Kocha wa United amesema: "Nafikiri
Schweinsteiger alimchezea rafu Wayne. Ilikuwa
ni kadi ya njano- au angalau faulo tu,".
Lakini United pia ilikuwa na bahati baada ya
kunusurika kumpoteza mchezaji mmoja,
kufuatia Antonio Valencia kuepuka kadi ya pili
ya njano kwa kumchezea rafu Jerome Boateng.
Moyes, pamoja na hayo, alimtetea mchezaji
wake kwa kusema: "Kijana aliufuata mpira
miguuni mwa Antonio Valencia,".
Mtu anajirusha, unatoa kadi: Pep Guardiola
akibishana na refa baada ya kadi nyekundu
Nenda nje: Carlos Velasco Carballo
akimuonyesha kadi nyekundu Schweinsteiger
Schweinsteiger alisawazisha bao la kuongoza la
United lililofungwa na Nemanja Vidic na
kuiweka Bayern katika nafasi nzuri ya
kushinda nyumbani ili kusonga mbele.
Lakini Moyes alionyesha ana imani kubwa
kwamba United inaweza kufika Nusu Fainali
katika msimu ambao imeshuhudiwa
wakisuasua katika Ligi Kuu ya England.
"Wakati wote nafikiri tutafunga bao dhidi yao
na nitakwenda Munich nikiamini tutafunga
goli,"alisema.
"Kuelekea kwenye mchezo huu, watu wengi
waliipa nafasi Bayern kushinda kwa urahisi,
wao ni mabingwa wa Ulaya. "Lakini usiku huu
tumeonyesha tunaweza kufika huko,
tutakwenda kula nao sahani moja ili
kuhakikisha tunawatoa,".
"Tunahitaji kufunga. Tunahitaji kwenda huko
kwa dhamira ya kushinda mechi. Timu
nyingine zimekwishakwenda huko na kufanya
hivyo, nasi tutahitaji kufanya hivyo
hivyo,"alisema Moyes jana.
TAZAMA PICHA ZA TUKIO LA KADI NYEKUNDU NINI MAONI YAKO

No comments:

Post a Comment