Wednesday, April 2, 2014
RAIS ROBERT MUGABE ASUSIA MKUTANO KUHUSU CAR.....
Viongozi wa Ulaya na Afrika wanatarajiwa
kuanza kujadili mgogoro unaotokota katika
Jamuhuri ya Afrika ya Kati, katika mkutano
maalum unaofanyika kando na kongamano
la viongozi wa Ulaya mjini Brussels.
Rais Robert Mugabe amesusia kongamano hilo
baada ya Muungano wa Ulaya kukataa
kumwondolea marufuku ya muda ya Visa
mkewe Grace.
Bwana Mugabe aliungwa mkono na Rais wa
Afrika Kusini Jacob Zuma, ambaye pia
ameamua kuususia mkutano huo kama ishara
ya kumuunga mkono Mugabe.
Zuma alisema kuwa muda umewadia wa Ulaya
kukoma kuwaangalia waafrika kama sio watu.
Muungano wa Ulaya tayari umezindua kikosi
cha jeshi lake nchini CAR, na kuelezea mipango
yake kutuma wanajeshi 1,000 kuwasaidia
wanajeshi wa Afrika na wale wa Ufaransa
wanaoshika doria nchini humo.
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa waisilamu
19,000 wanakabiliwa na tisho la kuuawa nchini
humo.
Maswala ya Uchumi na Uhamiaji pia yatapewa
kipaombele kwenye mkutano huo.
Viongozi 30 wanatarajiwa kuhudhuria
kongamano lenyewe wakiwemo marais wa
Afrika.
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-
moon atahudhuria mkutano kuhusu CAR
pamoja na viongozi wa Afrika na wale wa
Muungano wa Ulaya.
Ameahidi kufAnya kila awezalo kuhakikisha
anaimarisha juhudi za kukabiliana na migogoro
ya kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment