Tuesday, April 1, 2014

MICHEZO LEO: UCL: KITIMTIM NOU CAMP JUMANNE USIKU-BARCA v/s ATLETICO!..JUMANNE

Usiku Uwanja wa Nou Camp huko Jijini Barcelona utakuwa ndio
dimba la Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPIONZ
LIGI, UCL,
kati ya Barcelona na Atletico Madrid,Timu zote zikiwa toka Nchini Spain.Supastaa wa Barca, Lionel Messi, ataingia
kwenye Mechi hii akisaka kuvunja Rekodi ya Ufungaji inayoshikiliwa na Raul lakini yeye yuko bado Bao 4 pungufu kufikia Bao 71 na hii ni Mechi ngumu hasa kwa vile Barca na Atletico zilitoka 0-0
katika Mechi yao ya mwisho.

UEFA CHAMPIONZ LIGI WAFUNGAJI BORA 2013/14:
C. Ronaldo-Real Madrid Goli 13
Zlatan Ibrahimovic-PSG Goli 10
[Penati 1]
Messi-Barcelo na Goli 8 [Penati 2]
Diego Costa-Atletico Madrid Goli 7
Sergio Agüero-Manchester City Goli 6 [Penati 2]
Kwenye La Liga, Atletico ndio Vinara na Barca wako nyuma yao kwa Pointi 1 na Msimu huu
wameshakutana mara 3 na mara zote ni suluhu ingawa Barca walizoa Supercopa de Espana
Mwezi Agosti kwa Bao la Ugenini baada ya Sare ya Mechi zote mbili.Licha ya kulingana nguvu Msimu huu, Barca ndio wazoefu kwa Mechi za Ulaya na wameweza kufika Nusu Fainali za UCL
katika Misimu 6 iliyopita wakati Atletico wako kwenye Robo Fainali yao ya kwanza tangu Mwaka1997 na hawajatinga Nusu Fainali ya Michuano hii ya Ulaya kwa Miaka 40.Mara ya mwisho kwa Atletico kufika Robo Fainali ya Michuano hii, Miaka 17 iliyopita, Kocha wao
wa sasa, Diego Simeone,alikuwemo kwenye Kikosi kilichotolewa kwa Jumla ya Bao 4-3 na Ajax.Pia, Atletico hawajawahi kushinda Uwanjani
Nou Camp tangu Mwaka 2006 waliposhinda 3-1kwenye La Liga na Fernando Torres, ambae sasa
yuko Chelsea, kufunga Bao 2.Hata hivyo, Rekodi ya Barca dhidi ya Klabu nyingine ya Spain kwenye michuano ya Ulaya si nzuri baada kupoteza mara 5 kati ya 9 lakini
wamefungwa Mechi 1 tu kati ya 26 za Ulaya walizocheza mwisho Uwanjani kwao Nou Camp. Kila Timu itatinga kwenye Mechi hii ikiwakosa baadhi ya Wachezaji wao na Barca watamkosa
Kipa wao, Victor Valdes, ambae aliumia Goti hivi Juzi na atakuwa nje kwa Miezi 7.Atletico itacheza
bila ya Majeruhi Javier Manquillo na Raul Garcia ambae amefungiwa.

No comments:

Post a Comment