Madaktari katika hospitali kubwa zaidi ya umma nchini
Kenya,Kenyatta,wamefanikiwa kuondoa risasi iliyokuwa imekwama katika
ubongo wa mtoto Satrine Osinya mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.Risasi
hiyo iliyomuingia mtoto Satrine kichwani ndiyo iliyomuua mamake.Mamake
Satrine alikuwa amempakata
mtoto wake ili kumlinda kutokana na magaidi waliovamia kanisa walimokuwa
wiki moja iliyopita katika mtaa wa Likoni mjini Mombasa
.Lakini
walimpiga risasi mama huyo na kumuua papo hapo huku risasi iliyomuua
mama huyo ikiingia kichwani mwa Satrine na kukwama kwenye ubongo
wake.Satrine alipelekwa Nairobi kwa matibabu maalum kutoka Mombasa
kutokana na
ukosefu wa wataalamu wa upasuaji wa ubongo mjini humo.
Shughuli ya kuondoa risasi hiyo ilichukua saa tatu na ilifanywa na
madaktari watatu wakiongozwa Daktari Mwangi Gichuru ambaye ni mkuu wa
kitengo cha upasuaji
wa neva katika hospitali hiyo.
Matoto Satrine yuko salama na daktari Mwangi anasema hawakupata matatizo walipokuwa wanafanya upasuaji huo.
No comments:
Post a Comment