
Keshokutwa (Aprili 6 mwaka huu) kutakuwa na mechi kati ya Coastal na Mgambo Shooting Stars (Mkwakwani, Tanga), Oljoro JKT na Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid, Arusha), Rhino Rangers na Mtibwa Sugar (Ali Hassan Mwinyi, Tabora) na Yanga dhidi ya JKT Ruvu (Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam).Raundi hiyo itakamilika Aprili 9 mwaka huu kwa mechi kati ya Ruvu Shooting na Azam itakayochezwa Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani.
NI MWADUI AU STAND UNITED VPL MSIMU UJAO
Ni ipi kati ya timu za Mwadui na Stand
United, zote za Shinyanga itakayocheza Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) msimu
ujao itajulikana kesho (Aprili 5 mwaka huu) baada ya kundi C kuhitimisha
mechi za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu huu.Mwadui yenye pointi 28 ndiyo
inayoongoza, na itacheza na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Dodoma. Nayo Stand United yenye pointi 26 itaikaribisha Toto Africans
kwenye Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.Mechi nyingine zitakuwa kati ya Pamba na
Kanembwa JKT itakayochezwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza wakati
Polisi Mara na Polisi Tabora zitakwaruzana kwenye Uwanja wa Kumbukumbu
ya Karume mjini Musoma.Timu ambazo tayari zimepanda daraja kutoka FDL kucheza VPL msimu ujao ni Ndanda SC kutoka kundi A na Polisi Morogoro ya kundi B.
21 ZA KUCHEZA RCL ZAJULIKANA
Timu 21 kati ya 27 zitakazocheza Ligi ya
Mabingwa wa Mikoa (RCL) kutafuta tiketi ya kucheza Ligi Daraja la
Kwanza (FDL) msimu ujao tayari zimejulikana.
Timu hizo ni Abajalo SC (Dar es Salaam),
AFC (Arusha), African Sports (Tanga), Bulyanhulu FC (Shinyanga), Geita
Veterans (Geita), JKT Mafinga (Iringa), JKT Rwamukoma (Mara), Kariakoo
SC (Lindi), Kiluvya United (Pwani), Milambo SC (Tabora) na Mshikamano FC
(Dar es Salaam).
Nyingine ni Mvuvumwa FC (Kigoma), Navy
SC (Dar es Salaam), Njombe Mji (Njombe), Pachoto Shooting Stars
(Mtwara), Panone FC (Kilimanjaro), Singida United (Singida), Tanzanite
(Manyara), Town Small Boys (Ruvuma), Ujenzi FC (Rukwa) na Volcano
(Morogoro).
WATANO WAFANYA MTIHANI WA UWAKALA WA WACHEZAJI
Watanzania watano wamefanya mtihani wa
uwakala wa wachezaji wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA)
ambao ulifanyika jana (Aprili 3 mwaka huu) duniani kote.
Watahiniwa katika mtihani huo ambao
ulikuwa na maswali kutoka FIFA na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) walikuwa Godlisten Anderson, Jesse Koka, Lutfi Binkleb,
Rwechungura Mutahaba na Silla Yalonde.
VPL: LIGI KUU VODACOM
RATIBA:
Jumamosi Aprili 5
Kagera Sugar v Simba
Ashanti United v Mbeya City
Jumapili Aprili 6
Coastal Union v Mgambo JKT
JKT Oljoro v Tanzania Prisons
Rhino Rangers v Mtibwa Sugar
Yanga v JKT Ruvu
Jumatano Aprili 9
Ruvu Shooting v Azam FC
**RATIBA INAWEZA KUBADILIKA
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
MSIMAMO:
NA | TIMU | P | W | D | L | GD | PTS |
1 | Azam FC | 23 | 15 | 8 | 0 | 31 | 53 |
2 | Yanga SC | 22 | 13 | 7 | 2 | 26 | 46 |
3 | Mbeya City | 23 | 12 | 9 | 2 | 13 | 45 |
4 | Simba SC | 23 | 9 | 9 | 5 | 15 | 36 |
5 | Kagera Sugar | 22 | 8 | 9 | 5 | 3 | 33 |
6 | Mtibwa Sugar | 22 | 7 | 8 | 7 | 1 | 29 |
7 | Coastal Union | 23 | 6 | 11 | 6 | 0 | 29 |
8 | Ruvu Shooting | 21 | 7 | 8 | 6 | -4 | 29 |
9 | JKT Ruvu | 23 | 9 | 1 | 13 | -13 | 28 |
10 | Ashanti United | 22 | 5 | 6 | 11 | -17 | 21 |
11 | Mgambo JKT | 22 | 5 | 6 | 11 | -18 | 21 |
12 | Prisons FC | 22 | 3 | 10 | 9 | -10 | 19 |
13 | JKT Oljoro | 23 | 2 | 9 | 12 | -18 | 15 |
14 | Rhino Rangers | 23 | 2 | 7 | 14 | -19 | 13 |
**MSIMAMO HUU SI RASMI TOKA TFF
No comments:
Post a Comment