
Wakiwa wamebakisha Mechi 6 za Ligi Kuu England,Mourinho Leo anajitayarisha kuipokea Stoke City Uwanjani Stamford Bridge akijua fika ushindi tu ndio utawafanya waipiku Liverpool na kutwaa uongozi wa Ligi.Akiongelea Mechi hii, Mourinho amesema: “Sijui kama tutakuwa na uchezaji mzuri. Moja ya nguzo ya Timu za juu ni uimara wao. Lakini Timu yetu Msimu huu imekuwa ikipanda na kushuka.”Katika Mechi ya Kwanza iliyochezwa Desemba, Stoke City iliichapa Chelsea 3-2 katika Mechi ambayo Stoke walitoka nyuma na kufunga Bao la ushindi Dakika za Majeruhi kwa Bao la Oussama Assaidi, Mchezaji wa Mkopo kutoka Liverpool.Hivi sasa Ligi Kuu England inaongozwa na Liverpool wakiwa na Pointi 71 kwa Mechi 32 wakifuata Chelsea wenye Mechi 32 na Pointi 69, Man City ni wa 3 wakiwa na Mechi 30 Pointi 67 na Nafasi ya 4 ni Arsenal waliocheza Mechi 32 na wana Pointi 64.Pellegrini amesema, ingawa pambao lao na Liverpool Wikiendi ijayo ni muhimu, Ubingwa utaamuliwa mwishoni mwa Ligi.
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumamosi 5 Aprili 2014
1445 Man City v Southampton
1700 Aston Villa v Fulham
1700 Cardiff v Crystal Palace
1700 Hull v Swansea
1700 Newcastle v Man United
1700 Norwich v West Brom
1930 Chelsea v Stoke
LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili 6 Aprili 2014
1530 Everton v Arsenal
1800 West Ham v Liverpool
Jumatatu 7 Aprili 2014
2200 Tottenham v Sunderland
No comments:
Post a Comment