KLABU ya Manchester
United kuna hati hati ya kumkosa mshambuliajiwake mahiri Wayne Rooney
katikamchezo wa marudiano war obo fainali ya Ligi ya Mabingwa barani
Ulaya kwasababu ya kuumia kidole gumba. Mshambuliaji huyo wa kimataifa
wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28
alipata maumivu hayo Jumanne
iliyopita katika mchezo wa kwanza dhidi ya Bayern ambao walitoka sare ya
bao 1-1. Meneja wa United, David Moyes amesema nyota huyo ameumia
vibaya kidole gumba chake na inaweza kuwa tatizo katika mchezo wao dhidi
ya Bayern. Hata hivyo Moyes amesema watajitahidi kumpa matibabu yote
mwishoni mwa wiki na kuona kama anaweza kupona haraka kabla ya mchezo
wao wa Jumatano ijayo.
No comments:
Post a Comment