Saturday, April 5, 2014

JUAN MATA…NI MATATA, APIGA 2, AIBEBA MAN UNITED!

JUAN_MATA-13FEBWakicheza na Kikosi kilichobadilisha Wachezaji 8 toka kile kilichocheza Mechi yao ya mwisho Jumanne iliyopita walipotoka 1-1 na Bayern Munich kwenye Mechi ya Kwanza ya Robo Fainali ya UEFA CHAMPION LIGI, Man United wameitwanga Newcastle Bao 4-0 Ugenini Uwanja wa Saint James Park.United walifunga Bao lao la kwanza katika Dakika ya 38 kwa Frikiki ya Juan Mata.
Hilo ni Bao la Pili la Mata kwa Man United tangu ahamie hapo Mwezi Januari na la Kwanza alifunga Wikiendi iliyopiita Man United walipoifunga Aston Villa.Mata, ambae ndie alieng’ara sana Mechi hii, alifunga Bao lake la Pili na la Pili kwa Man United,katika Dakika ya 50 kufuatia muvu kali iliyowahusisha Shinji Kagawa na Chicharito.Javier Hernandez Chicharito, alipiga Bao la 3 katika Dakika ya 65, kutokana na kazi njema ya Adnan Januzaj na Shinji Kagawa.Bao la 4 lilifungwa na Adnan Januzaj, katika Dakika ya 90, na hii tena ilikuwa muvu kali ambayo Mata alihusika.
VIKOSI:

NEWCASTLE: Newcastle United: Elliot; Santon, Williamson, Coloccini, Haidara; Anita, Gosling, Tiote, Gouffran; de Jong, Cissé.

Akiba: Alnwick, S.Taylor, Yanga-Mbiwa, Dummett, Ben Arfa, Shola Ameobi, Armstrong.
MAN UNITED: Lindegaard; Valencia, Jones, Smalling, Evra; Young, Mata, Fletcher, Fellaini, Kagawa; Hernandez ‘Chicharito’

Akiba: De Gea, Büttner, Vidic, Cleverley, Januzaj, Nani, Wilson 
REFA: Kevin Friend

CITY NI YA PILI, POINTI 1 NYUMA YA LIVERPOOL NA MECHI MKONONI!

 NASRI_APIGA_BAO_LA_PILIManchester City, wakiwa kwao Etihad, katika Mechi ya Kwanza kabisa hii Leo ya Ligi Kuu England, wameonyesha azma yao ya Ubingwa baada ya kuitandika 4-1 Southampton inayotandaza Soka safi.Manchester City walitangulia kupata Bao kwa Penati ya Yaya Toure ya Dakika ya 3 tu na Penati hiyo ilitolewa na Refa Chris Foy baada Beki Jose Fonte kumwangusha Edin Dzeko.Hilo lilikuwa Bao la 22 kwa Toure Msimu huu.Dakika ya 37 Rickie Lambet alisawazisha kwa Southampton kwa Penati iliyolewa na Refa Chris Foy kwa Rafu ya Pablo Zabaleta kwa Jack Cork.Wakati Bango linaashiria Dakika za Nyongeza 4 kabla Mapumziko, Man City walifunga Bao lao la pili baada ya muvu safi kati ya Samir Nasri aliempa Yaya Toure kumpa Edin Dzeko alierudisha kwa kisigino kwa David Silva ambae alirudisha Samir Nasri aliemchambua Kipa Paulo Gazzaniga.Dakika moja baadae, Samir Nasri tena alianza muvu kwa kumpelekea Aleksandar Kolarov kwenye Winga ya Kushoto ambae alimimina Krosi murua iliyomaliziwa kwa kichwa na Edin Dzeko na kuifanya Man City iende Haftaimu ikiwa Bao 3-1 kwa mbele.Dakika ya 81, Stevan Jovetic, alieingizwa Dakika chache kumbadili David Silva, aliifungia Man City Bao lao la 4 alipounganisha Krosi ya chini kutoka upande wa kulia ya Jesus Navas na ambayo ilikoswa na Alvaro Negredo huku Kipa Gazzaniga akiwa hayupo mstarini.Ushindi huu umeipandisha Man City na kuwa Nafasi ya Pili Pointi 1 nyuma ya Liverpool na pia wana Mechi 1 mkononi.
VIKOSI:
MANCHESTER CITY: Hart, Zabaleta, Kompany, Demichelis, Kolarov, Toure, Fernandinho, Jesus Navas, Silva, Nasri, Dzeko.
Akiba: Richards, Lescott, Milner, Negredo, Javi Garcia, Pantilimon, Jovetic.
SOUTHAMPTON: Gazzaniga, Chambers, Lovren, Fonte, Shaw, Schneiderlin, Cork, Lallana, Steven Davis, Rodriguez, Lambert.
Akiba: Wanyama, Ward-Prowse, Do Prado, Hooiveld, Gallagher, Cropper, Clyne.
Refa: Chris Foy

ASTON VILLA 1 FULHAM 2 
-Villa Park
Hadi Mapumziko, Bao zilikuwa 0-0 lakini Kieran Richardson akawapa Fulham Bao la kuongoza katika Dakika ya 61 na Grant Holt kusawazisha Dakika ya 70 na Bao la ushindi kufungwa na Hugo Rodallega, alietokea Benchi, katika Dakika ya 86.
Ushindi huu umefufua matumaini ya Fulham kuweza kubakia Ligi Kuu England.
VIKOSI:
Aston Villa: Guzan, Lowton, Vlaar, Baker, Bertrand, Westwood, Bennett, Bacuna, Albrighton, Weimann, Holt
Akiba: Steer, Sylla, Tonev, Clark, Robinson, Luna, Bowery.
Fulham: Stockdale; Riether, Hangeland, Heitinga, Amorebieta; Diarra, Sidwell; Kasami, Holtby, Richardson; Woodrow
Akiba: Stekelenburg, Riise, Kvist, Kacaniklic, Rodallega, Dejagah, Roberts. 
Refa: Michael Oliver.

CARDIFF CITY 0 CRYSTAL PALACE 3
-Cardiff City Stadium
Jason Puncheon alifunga Bao mbili, Dakika ya 31 na 88, na Joe Ledley kupiga Bao moja katika Dakika ya 71 na kuwapa Palace ushindi wa Bao 3-0 wakicheza Ugenini na Cardiff City ambayo sasa ipo kwenye hatari kubwa kushuka Daraja.
VIKOSI:
Cardiff City: Marshall; Theophile-Catherine, Caulker, Turner, Taylor; Medel, Mutch, Daehli, Zaha; Campbell, Jones
Akiba: Lewis; Eikrem, Noone, Cowie, Mcnaughton, Cala, Bellamy.
Crystal Palace: Speroni, Mariappa, Dann, Delaney, Ward, Dikgacoi, Jedinak, Ledley, Puncheon, Bolasie, Jerome
Akiba: Hennessey, Gabbidon, Parr, Ince, Gayle, Murray, Chamakh.
Refa: Phil Dowd.

HULL CITY 1 SWANSEA CITY 0
-KC Stadium
George Boyd ndie alieifungia Hull City Bao lao katika Dakika ya 39.
VIKOSI:
Hull City: Harper, Rosenior, Figueora, Chester, Davies, Meyler, Livermore, Boyd, Jelavic, Long, Elmohamady
Akiba: Jakupovic, Bruce, Koren, Fryatt, Sagbo, Aluko, Quinn.
Swansea City: Vorm, Rangel, Chico Flores, Williams , Davies, Britton, Shelvey, De Guzman, Routledge, Michu, Bony
Akiba: Tremmel, Taylor, Amat, Canas, Hernandez, Dyer, Lita.
Refa: Martin Atkinson.

NORWICH CITY 0 WEST BROMWICH ALBION 1
-Carrow Road
Amalfitano ndie aliewapa WBA Bao lao ushindi katika Dakika ya 16.
VIKOSI:
Norwich City: Ruddy; Martin, Yobo, Bassong, Olsson; Snodgrass, Howson, Tettey, Hoolahan; Elmander, Hooper
Akibs: Bunn, Whittaker, Johnson, van Wolfswinkel, Gutierrez, Becchio, Redmond.
West Bromwich Albion: Foster, Reid, McAuley, Olsson, Ridgewell, Amalfitano, Morrison, Mulumbu, Dorrans, Sessegnon, Vydra
Akiba: Myhill, Thievy, Berahino, Dawson, O’Neil, Gera, Anichebe.
Refa: Mark Clattenburg

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA/MATOKEO:
Jumamosi 5 Aprili 2014
Man City 4 Southampton 1 
Aston Villa 1 Fulham 2
Cardiff City 0 Crystal Palace 3
Hull 1 Swansea 0
Newcastle 0 Man United 4
Norwich 0 West Brom 1
[Saa za Bongo]
1930 Chelsea v Stoke

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumapili 6 Aprili 2014
1530 Everton v Arsenal
1800 West Ham v Liverpool
Jumatatu 7 Aprili 2014
2200 Tottenham v Sunderland 

MSIMAMO:
NA TIMU P W D L F A GD PTS
1 Liverpool 32 22 5 5 88 39 49 71
2 Manchester City 31 22 4 5 84 29 55 70
3 Chelsea 32 21 6 5 62 24 38 69
4 Arsenal 32 19 7 6 56 37 19 64
5 Everton 31 17 9 5 49 31 18 60
6 Manchester United 33 17 6 10 56 38 18 57
7 Tottenham Hotspur 32 17 5 10 40 44 -4 56
8 Southampton 33 13 9 11 50 44 6 48
9 Newcastle United 33 14 4 15 38 51 -13 46
10 Stoke City 32 10 10 12 37 45 -8 40
11 West Ham United 32 10 7 15 36 42 -6 37
12 Hull City 33 10 6 17 34 40 -6 36
13 Aston Villa 32 9 7 16 35 48 -13 34
14 Crystal Palace 32 10 4 18 23 39 -16 34
15 Swansea City 33 8 9 16 45 49 -4 33
16 West Bromwich Albion 32 6 14 12 37 48 -11 32
17 Norwich City 33 8 8 17 26 52 -26 32
18 Fulham 33 8 3 22 33 74 -41 27
19 Cardiff City 33 6 8 19 29 64 -35 26
20 Sunderland 30 6 7 17 28 48 -20 25
++++++++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA MECHI ZIJAZO:
[Saa za Bongo]
Jumamosi 12 Aprili 2014
1700 Crystal Palace v Aston Villa
1700 Fulham v Norwich
1700 Southampton v Cardiff
1700 Stoke v Newcastle
1700 Sunderland v Everton
1700 West Brom v Tottenham
Jumapili 13 Aprili 2014
1530 Liverpool v Man City
1800 Swansea v Chelsea
Jumanne 15 Aprili 2014
2145 Arsenal v West Ham
Jumatano 16 Aprili 2014
2145 Everton v Crystal Palace
2145 Man City v Sunderland

No comments:

Post a Comment