mwaka 2001 kwa sababu alimbiwa
na Mungu asioge Nadhani ulishawahi kusikia ama kushuhudia watu wa eneo Fulani ama jamii fulani wakimlazimisha kichaa kuoga kwa nguvu kwa
kuwa amezidi kuwa mchafu, lakini hii ni tofauti kwa waumini wa dhehebu analolisimamia mchungaji Wale Olanguji wa
Nigeria.Mchungaji Wale wa kanisa la Divine Seed of God wa Ibadan, Oyo, Nigeria ameliambia jarida la People City la Nigeria kuwa hajawahi kuoga tangu mwaka 2001 wakati ambapo anadai alipokea amri ya Mungu ikimtaka
afanye hivyo na kwamba ajitenge na mkewe na kuacha kutumia baadhi ya vinywaji.Cha ajabu, licha ya kukaa miaka 13 bila kuoga
mchungaji huyo hatoi harufu na ni vigumu kumshitukia hadi akuoneshe mwenyewe
vielelezo! Hivi ndivyo mchungaji huyo alivyoliambia jarida hilo wakati lilipomkumbusha kuwa
mwaka 2001 alitoa maelezo kuwa Mungu amemwambia asioge:
"Ndiyo, ni miaka 13 hadi sasa kwa ufupi.Mwaka 2000 mwanzoni Mungu aliniambia niache kuoga, nijitenge na mke wangu na
kwamba natakiwa kuacha kutumia vinywaji vyote laini pamoja na wines. Na tangu wakati
huo…kwa kweli, nimekuwa nikifuata yote hayo."Mtu yeyote ambaye Mungu anataka
kumtumia kwa sababu hapa duniani, kuna gharama imeambatanishwa kwenye huo wito.Kwa hiyo ninaamini kwamba hiyo ni gharama ninayolipa. Ninavyoongea na wewe hivi sasa,
sijaoga, kama unataka nikuoneshe ushahidi
nitakuonesha kama una shaka juu ya haya yote nisemayo; sijaoga tangu mwaka 2001 hadi
wakati huu."
No comments:
Post a Comment