Thursday, April 3, 2014

MAN WATER AJIVUNIA KUFANYA KAZI NA JIDE....

MTAYARISHAJI mahiri wa muziki kutoka Studio ya Combination Sounds,John Shariza ‘Man Water' amefunguka kuwa kufanya kazi na mwanadada Judith Wambura ‘Jide’kumemsogeza mbele katika muziki wake na kimaisha.Man Water, ametengeneza kazi mbili za mwanadada huyo zinazofanya vizuri katika soko la muziki,ambazo ni ‘Joto Hasira’ na ‘Yahaya’.Akizungumza jijini Dar es Salaam,Man Water alisema kufanya kazi na msanii mkongwe na ukafanikiwa kufuata kile anachokitaka yeye inakuwa ni faraja sana.
Pia alisema kuwa ameweza kujiamini anaweza kufanya maajabu zaidi, kwa sababu ilikuwa ni ndoto kufanya kazi na Jide na alikuwa anatamani sana. “Nashukuru Mungu amesikia kilio changu, nafikiri kazi nzuri niliyoifanya imenifanya niingie katika kinyang’anyiro cha mtayarishaji bora katika tuzo za Kili, naombeni wapenzi wangu msinisahau katika hili,”alisema.Alisema bado ana mikakati yakufanya kazi na Jide, kwani kutokana na kufanya naye kazi vizuri,ametokea kumuamini.Mbali na hilo, mtayarishaji huyo alisema kuwa, pia amefanya kazi nzuri ya Christian Bella aliyomshirikisha Ommy Dimpoz.

No comments:

Post a Comment