Wanajeshi wanne wamepigwa risasi na kuuawa
katika kambi ya jeshi huko Fort Hood jimboni Texas. Jenerali Mark
Milley, amesema mwanajeshi mmoja ndiye aliyewafyetulia wenzake risasi
hizo karibu na zahanati ya afya ya kijeshi ya Carl R Darnall iliyoko
katika kambi hiyo ya Jeshi.Watu watatu walifariki kabla ya mwanajeshi huyo kujipiga risasi na kujiua.Wanajeshi wapato wannewanatibiwa majeraha mabaya ya risasi.
Daktari mkuu wa zahanati hiyo Dakta Glen Couchman
anaelezea majeraha wanayotibu.''Wote walikuwa na majereha mbalimbali ya
risasi kwenye vifua shingo na tumbo''.Mauaji katika kambi ya Jeshi Marekani Waziri wa usalama Chuck Hagel amesema kuwa uchunguzi tayari umeshaanza kubaini chanzo cha kisa hicho cha pili
kuikumba kambi hii. ''ninajua kuwa mtangulizi wangu Leon Pannetta
aliwahi kusema kuwa tukio kama hili mwaka wa 2009 litachunguzwa.Ni wazi lazima kuna kitu kinachoendelea ambacho hakifai.
Lazima tutatue shida hii .''Rais Obama amehuzunishwa sana na tukio hilo
ambalo anasema limetokea katika kambi ambayo inapaswa kuwa salama .Obama
amesema ''amezungumza na maafisa wa FBI na idara ya mahakama kutafuta
kwa kina kiini cha makabiliano haya ilikuhakikisha kambi zetu zimekuwa salama. Hii siyo mara ya kwanza kwa kituo hicho kikubwa cha majeshi ya Marekani Fort Hood kushuhudia ufyetulianaji wa
risasi .Mwaka 2009 wakati dakatari wa magonjwa ya kiakili wa jeshi la
Marekani meja Nidal Hasan
alipowapiga risasi na kuwaua watu kumi na watatu.Rais Obama amesema anafuatilia yanayotukia katika kambi hiyo kwa makini.
No comments:
Post a Comment