
Wiki
chache zilizopita mwanamuziki Shakira alikaririwa akisema kwamba
mchumba wake ambaye ni mwanasoka wa klabu ya FC Barcelona Gerard Pique
amemkataza kuendelea kufanya video na models wa kiume. Kauli hiyo ya
Shakira ambaye anatamba na ngoma yake ya ‘Cant Remember to Forget You’
ilitengeneza vichwa vya habari vingi sana.
Sasa ikiwa zimepita siku kadhaa mwanamuziki huyo raia wa Colombia
jana alitumia mtandao wa Facebook kupitia akaunti yake rasmi na kusema
kwamba alikuwa anatania na sio kweli kwamba Pique amemkataza
kushirikiana na models wa kiume kwenye videos zake.
No comments:
Post a Comment