Bwana Misosi aliyetamba zamani na wimbo
wake wa MABINTI WA KITANGA atoa taarifa baada ya account yake kuingia mikononi mwa wajanja (Hackers),Story ipo hiviiiii........
Misosi alipata ujumbe kutoka kwa mtu akimlazimisha abonyeze link ambayo
ilianza na maneno ya kuwa ameandikwa vibaya kwa habari kamili bonyeza
hiyo link. Misosi akabonyeza wakati anaendelea ukaja ujumbe eti aingize
email yake na password ili auone huo upuuzi, basi ndugu yetu akaingiza
mwisho wa siku jamaa wakaendelea kufanya yao. Sasa Bw Misosi anawaomba
mashabiki wake kutoingia kwenye account yake hii https://www.facebook.com/bwana.misosi.1?fref=ts au ukiona vitu vya upuuzi usiamini kuwa ni yeye.Ushauri wangu wa bure kwa wasanii wa hapa
nyumbani msipende kubonyeza bonyeza link mtakazotumiwa yasije kuwakuta
kama yaliyomkuta ndugu yetu Bw. Misosi. Kuna link na link unaweza
kubonyeza sasa mpaka link hii inasema weka email yako na Password bado
tu unaendelea kujaza mmmmh hii ni zaidi ya noma.
No comments:
Post a Comment