Monday, April 28, 2014

DEL PIERO AAMUA KUTUNDIKA DARUGA.

MCHEZAJI mkongwe Alessandro Del Piero ameamua kutundika daruga kuitumikia klabu ya Sydney FC lakini anaweza kurejea kwa shughuli nyingine. Nguli huyo wa zamani wa Juventus amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa kocha katika klabu hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchiniAustralia maarufu kama A-League baada ya Frank Farina kutimuliwa.

WACHEZAJI WA LOS ANGELES CLIPPERS WAFANYA MAANDAMANO YA KIMYA KIMYA KUFUATIA KAULI YA KIBAGUZI YA BOSI WAO.

WACHEZAJI wa mpira wa kikapu nchini Marekani wamefanya maandamano ya kimya kimya kufuatia ripoti kuwa mmiliki wa timu yao amerekodiwa kisiri akitoa kauli za kibaguzi. Los Angeles Clippers waliingia kupasha misuli moto jana huku fulana zao wakiwa wamezigeuza ndani-nje ili kuficha nembo ya timu hiyo. 

KLABU AFRIKA: DROO ZA MAKUNDI KUFANYIKA JUMANNE!


DROO za kupanga Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho itafanyika Jumanne Aprili 29 huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini Misri.Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI zipo Timu 8 zilizofuzu hatua hii na Droo hiyo itapanga Makundi mawili ya Timu 4 kila moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi,

UEFA CHAMPIONS LIGI: FAINALI, NI MABINGWA BAYERN AU REAL WANAOSAKA ‘DECIMA’?



FC Bayern Munich v Real Madrid CF
-Allianz Arena, Munich, Germany
HILI ni pambano kali sana na Mabingwa Watetezi, Bayern Munich, chni ya Meneja wao Pep Guardiola, ambae anaifahamu fika Real Madrid tangu enzi zake akiwa na Barcelona, ana kazi nzito ya kugeuza kipigo cha Bao 1-0 ili watinge Fainali.Kihistoria, Bayern Munich wana Rekodi nzuri sana dhidi ya Real Madrid wakiwa kwao huko Munich lakini kwenye Mechi hizi Historia huwa inabaki Vitabuni tu na kuandikwa baada ya Mechi.

PFA-TUZO YA MCHEZAJI BORA WA MWAKA: NI LUIS SUAREZ!

STRAIKA wa Liverpool Luis Suarez ametwaa Tuzo ya England ya Mchezaji Bora wa Mwaka ya PFA [Professional Footballers' Association], Chama cha Wanasoka wa Kulipwa, hapo Jana.Msimu uliopita, kipindi kama hiki, Luis Suarez alikuwa akianza kutumikia Adhabu ya Kifungo cha Mechi 10 baada kumuuma Meno Mchezaji wa Chelsea, Branislav Ivanovic,