DROO za kupanga Makundi ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Kombe la Shirikisho itafanyika Jumanne Aprili 29 huko Makao Makuu ya CAF Jijini Cairo Nchini Misri.Kwenye CAF CHAMPIONZ LIGI zipo Timu 8
zilizofuzu hatua hii na Droo hiyo itapanga Makundi mawili ya Timu 4 kila
moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi,
Nyumbani na Ugenini, ili kupata
Timu mbili za juu toka kila Kundi kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
-Al-Ahly Benghazi ya Libya
-Al-Hilal ya Sudan
-AS Vita Club ya Congo DR
-CS Sfaxien ya Tunisia
-Espérance de Tunis ya Tunisia
-ES Sétif ya Algeria
-TP Mazembe ya Congo DR
-Zamalek ya Egypt
Mechi za Makundi zitaanza Wikiendi ya Mei 16 hadi 18.
CAF Kombe la Shirikisho
Kwenye CAF Kombe la Shirikisho, Droo ya
hapo kesho Jumanne pia itashirikisha Timu 8 ambazo nazo zitagawanywa
Makundi mawili ya Timu 4 kila moja ambayo yatacheza mtindo wa Ligi,
Nyumbani na Ugenini, ili kupata Timu mbili za juu toka kila Kundi
kucheza Nusu Fainali.
Timu hizo 8 ni:
-Sewe Sport - Ivory Coast
-Al Ahly – Egypt
-AS Real de Bamako – Mali
-AC Leopards de Dolisie – Congo
-ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast
-Coton Sport FC – Cameroon
-E.S. Sahel – Tunisia
Mechi za Makundi zitaanza Wikiendi ya Mei 16 hadi 18.
CAF Kombe la Shirikisho
Marudiano
[Kwenye Mabano Jumla ya Mabao kwa Mechi mbili]
Jumamosi Aprili 26
Bayelsa United – Nigeria 0 Sewe Sport - Ivory Coast 1 [0-3]
Difaa Hassani El Jadidi – Morocco 2 Al Ahly – Egypt 1 [2-2, Al Ahly yasonga kwa Bao la Ugenini]
Jumapili Aprili 26
Djoliba AC – Mali 0 AS Real de Bamako – Mali 0 [1-2]
Medeama – Ghana 2 AC Leopards de Dolisie – Congo 0 [2-2, Penati 4-5]
ASEC Mimosas Abidjan - Ivory Coast 1 Kaizer Chiefs - South Africa 0 [3-1]
Petro Atlético de Luanda - Angola 2 Coton Sport FC – Cameroon 2 [3-4]
E.S. Sahel – Tunisia 1 Horoya Athlétique Club – Guinea 0 [1-0]
C. A. Bizertin – Tunisia 1 Nkana FC – Zambia 1 [1-1]

No comments:
Post a Comment