MCHEZAJI mkongwe
Alessandro Del Piero ameamua kutundika daruga kuitumikia klabu ya Sydney
FC lakini anaweza kurejea kwa shughuli nyingine. Nguli huyo wa zamani
wa Juventus amekuwa akihusishwa na tetesi za kuwa kocha katika klabu
hiyo inayoshiriki Ligi Kuu nchiniAustralia maarufu kama A-League baada
ya Frank Farina kutimuliwa.
Del Piero mwenye umri wa miaka 39 na klabu
hiyo wanataka kuendelea na mahusiano lakini haijabainika wazi ni
uhusiano wa namna gani. Baada ya kufunga mabao 24 ambayo yamemfanya
kumaliza kama mfungaji bora wa klabu katika misimu yote miwili
aliyoitumikia, Del Pierro ametoa ujumbe wa kushukuru na kuaga
katikamtandao wake. Del Piero amesema katika ujumbe huo ule wakati
umewadia safari yake akiwa na Sydney FC inakaribia ukingoni ingawa
inasikitisha lakini amekuwa na muda mzuri katika kipindi chote
alichoitumikia.

No comments:
Post a Comment