Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba linaahirishwa
leo baada ya kukutana kwa siku 67 bila kupitisha hata ibara moja kati ya
240 zilizomo katika Rasimu ya Katiba.Badala yake Bunge hilo likiongozwa na Samuel Sitta
“Mzee wa Kasi na Viwango” linaahirishwa hadi Agosti, mwaka huu
likiendelea kujadili Sura ya Kwanza
na ya Sita zenye jumla ya Ibara 19, zinazohusu masuala yanayojenga msingi wa aina ya Muungano unaopendekezwa.
Tume ya Mabadiliko ya Katiba katika rasimu iliyowasilishwa bungeni na aliyekuwa Mwenyekiti wake, Jaji Joseph Warioba ilipendekeza muundo wa shirikisho lenye serikali tatu, pendekezo ambalo limeligawa Bunge hilo vipande viwili.Kutokana na mgawanyiko huo, kauli zenye utata, kejeli, matusi, dhihaka na ubaguzi ni mambo yaliyoshika hatamu katika mjadala wa sura hizo mbili, huku viongozi wa Bunge; Sitta na Makamu wake, Samia Suluhu Hassan wakilaumiwa kwa kushindwa kudhibiti hali hiyo.

Mwanzoni mwa wiki hii, Mjumbe wa Bunge hilo,
Ezekiah Oluoch alimshutumu Sitta kwamba ameshindwa kudhibiti nidhamu
katika Bunge na kwamba ndiye chanzo cha kuondoka kwa wajumbe wapatao 200
ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).“Mwenendo wa Bunge Maalumu ulikuwa na dalili zote
za kuonyesha kungetokea matatizo ndani yake kutokana na mipasho ambayo
ilikuwa ikitokea kwa wajumbe pamoja na lugha ambazo siyo za staha wakati
wa kutengeneza kanuni,” alisema Oluoch na kuongeza:“Kwanza matumizi ya lugha zisizo na staha,
mwenyekiti anaruhusu wajumbe kuchangia hoja kwa kupeana mipasho bila
kujali hoja iliyopo mezani kinyume na kanuni,” alisema Olouch.
Hata hivyo, Suluhu alisema amekuwa akiendesha
Bunge hilo kwa umakini mkubwa na kwamba kila anaposikia lugha chafu
amekuwa akiwabana wajumbe kwa kuwaamuru kufuta kauli au kuomba radhi kwa
matamshi. “Sipendezwi na lugha chafu, kwa hiyo mojawapo ya mambo ambayo
huwa najitahidi kusikiliza kwa makini kila michango inapotolewa na
wajumbe bungeni ni kubaini kama wametumia lugha zisizostahili, kisha
kuchukua hatua kwa mujibu wa kanuni zetu,” alisema Suluhu.Alikiri kwamba wapo baadhi ya wajumbe ambao
wamekuwa wakigoma au kukataa kuomba radhi na kwamba masuala yao
hupelekwa kwenye Kamati ya Maadili ambayo ina mamlaka ya kuchukua hatua
zaidi kwa mujibu wa kanuni za Bunge hilo.

No comments:
Post a Comment