Saturday, April 26, 2014

NISSAN WAJA NA KALI....."GARI INAYOJIOSHA YENYEWE"

      
Kampuni kubwa ulimwenguni inayotengeneza Gari aina ya Nissan,imetoa toleo jipya ya Nissan-Note yenye uwezo wa kujiosha yenyewe.....video hii ikithibitisha
hilo=>https://www.youtube.com/watch?feature=player_embedded&v=UwoGsCAKsxU#t=5
Sasa naona Nissan wameamua kumvuruga kichwa mshkaji wangu Jaffarai, na gari lao jipya lenye uwezo wa kujisafisha lenyewe, yaani hakuna kuosha gari kabisa.usishtuke sana bwana Jaffarai, Nissan walaaaa, wanafanya yao tu, ila licha ya kuwa ni gari kali, lakini siwezi kuliita gari linalojiosha lenyewe (mtanisamehe Nissan) bali ni gari ninaloweza kusema halishiki uchafu wa aina yoyote, na hata hiki kipande cha video kilichotolewa na Nissan kinathibitisha hili.Nissan wameanzisha rangi isiyoruhusu. vumbi, matope, uchafu wala maji kubaki kweye body ya gari na kuiacha gari ikiwa ina ng'ara bila ya kuiosha wala kuifuta. Kwa mujibu wa Nissan rangi hiyo inazuia maji na mafuta pia, na ubunifu huo ulifanikiwa kwa "kutengeneza tabaka la kinga ya hewa kati ya rangi na mazingira".Rangi hiyo inaitwa Ultra-Ever Dry na imetengenezwa na UltraTech International Inc.gari hili la majaribio linaonyesha upande wa kulia uliopakwa rangi hiyo na upande wa kushoto wenye rangi ya kawaida.

No comments:

Post a Comment