Wednesday, April 2, 2014

BARCELONA YAFUNGIWA KUSAJILI NA FIFA.

KLABU ya Barcelona imefungiwa kusajili
wachezaji kwa vipindi viwili vya usajili na
Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kukiuka
taratibu za kimataifa zinazohusu usajili wa
wachezaji chini ya umri wa miaka 18. Hatua
hiyo imekuja kufuatia uchunguzi wa awali
uliofanywa na shirikisho hilo kupitia mfumo
wake wa uhamisho-TMS kwa mwaka
uliopita
. Barcelona wamekutwa wamekiuka
vifungu kadhaa kuhusiana na uhamisho wa
kimataifa sambamba na usajili wa wachezaji
walio chini ya umri ambao sio raia wa
Hispania. Uchunguzi huo ulihusisha wachezaji
kadhaa walio chini ya umri huo ambao
waliandikishwa na kushiriki mashindano
wakiwa na timu hiyo katika kipindi cha mwaka
2009-2013.

No comments:

Post a Comment