Wednesday, April 2, 2014

BAADA YA JANA USIKU MANCHESTER UNITED KUWADINDIA BAYERN MUNICH KWA KUTKA SARE YA GORI 1-1 KIMBEMBE LEO MACHINJIONI': BERNABEU KWA REAL..NA..PARC DES PRINCES KWA PSG!

#UEFA CHAMPIONS LEAGUE ‘MACHINJIONI’:BERNABEU KWA REAL,,,,,PARC DES PRINCE
KWA PSG! UEFA CHAMPIONZ LIGI
ROBO FAINALI
 Jumatano Aprili 2 ,,,Real Madrid v/s Borussia Dortmund
Paris Saint-Germain v Chelsea
BAADA Robo Fainali za UEFA CHAMPIONZ LIGI,UCL, kuanza kunguruma Jumanne Aprili
Mosi kwa Mechi mbili kati ya Manchester United na
Mabingwa Watetezi, Bayern Munich na ile ya Klabu za Spain, Barcelona v Atletico Madrid,Mechi za Kwanza zitakamilika Jumatano Usiku kwa Mechi mbili ambapo huko Santiago Bernabeu, Jijini Madrid, Real Madrid wataivaa

Borussia Dortmund na huko Parc des Princes,Jijini Paris, France, Paris Saint-Germain itakumbana na Chelsea.Marudiano ya Mechi zote hizi ni Wiki ijayo.

PATA RIPOTI ZA MECHI HIZO:
REAL MADRID v BORUSSIA
DORTMUND..Msimu uliopita, Timu hizi zilikutana kwenye Nusu Fainali ya Mashindano haya na Dortmund ndio waliotoka kidedea hasa baada ya kuitwanga Real Madrid Bao 4-1 katika Mechi ya Kwanza na kufungwa Bao 2-0 kwenye Marudiano huko Santiago
Bernabeu na hivyo kusonga Fainali kwa Jumla ya Bao 4-3.
Kwenye Mechi hiyo ya Kwanza, Straika Robert Lewandowski ndio alieibeba Dortmund kuiua
Real.Lakini tangu wakati huo mambo mengi yamebadilika na Real wana Meneja mpya,
Carlo Ancelotti, na Wachezaji wapya, Gareth Bale na Isco, wakati Dortmund washamuuza
Staa wao Mario Gotze kwa Bayern Munich na Msimu huu wamekuwa wakisuasua na kukabiliwa na Majeruhi wengi kwenye Kikosi chao.Chini ya Carlo Ancelotti, Real walipiga
mwendo wa Mechi 31 bila kufungwa kati ya Oktoba 13
na Machi 23 na kisha kufungwa Mechi 2 mfululizo hivi Majuzi mikononi mwa Barcelona na Sevilla.Lakini Real hawajafungwa kwenye UCL tangu wapigwe
hizo Bao 4-1 na Dortmund Uwanjani Signal Iduna Park Msimu uliopita na Msimu
huu,Raundi iliyopita ya UCL, wameitoa Schalke inayocheza Bundesliga pamoja na Dortmund.

MECHI 3 ZILIZOPITA KATI YA REAL NA DORTMUND:
-Real Madrid 2 (Benzema, Ramos) Dortmund 0,UCL, Aprili 30, 2013
-Dortmund 4 (Lewandowski 4) Real Madrid 1(Ronaldo), UCL, Aprili 23, 2013
-Real Madrid 2 (Pepe, Ozil) Dortmund 2 (Reus,Arbeloa Kajifunga mwenyewe), UCL,
Novemba 2012

PARIS SAINT-GERMAIN v CHELSEA
Chini ya Nahodha wa zamani wa France,Laurent Blanc, ambae pia aliwahi kuichezea Man United, Paris St-Germain,inaanza kujengeka na kuwa Timu inayoogopewa Barani Ulaya huku Straika wao, Zlatan Ibrahimovic, akiwa ni tishio kubwa na Msimu
huu ameshapachika Bao 40 na kupitwa tu na Mchezaji Bora Duniani, Cristiano Ronaldo.
Baada ya kushtukizwa na kufungwa Bao 1-0 na Crystal Palace Jumamosi iliyopita kwenye Ligi Kuu England, na kipigo hicho kinafuatia kile toka kwa Aston Villa, kimeyaacha matumaini
ya Chelsea kutwaa Ubingwa kufifia na sasa nguvu zao zipo Ulaya.Lakini Chelsea wana kibarua kigumu mno kwani PSG wapo katika mwendo wa kutofungwa Mechi 13 na hawajafungwa Nyumbani kwao, Parc des Princes, katika Mechi 9 za UCL wakati Chelsea wameshinda Mechi 1 tu kati ya 6 walizocheza mwishoni Ugenini kwenye
UCL.MECHI MBILI ZILIZOPITA KATI YA CHELSEA NA PSG:
-Chelsea 0 Paris St-Germain 0, UCL,Novemba 2004
-Paris St-Germain 0 Chelsea 3 (Terry, Drogba 2),UCL, Septemba 2004

No comments:

Post a Comment